HEADLINES

6/recent/ticker-posts

UVCCM KUZINDUA JAMBO KUBWA LA VIJANA UWANJA WA MKAPA JUMAMOSI HII


Na AMEDEUS SOMI,
DAR ES SALAAM.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi UVCCM Jokate Mwegelo ametangaza uzinduzi wa Kampeni maalum ya kujadili fursa mbalimbali kwa vijana zilizotengenezwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan.


Uzinduzi huo utaongozwa na Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Balozi Dkt.Emmanuel Nchimbi, Mwenyekiti wa UVCCM Taifa Mohammed Kawaida na Naibu Aibu Mkuu wake Rehema Sombi.


Aidha Mwegelo ametumia fursa hiyo kuwahimiza vijana kujitokeza kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura linalotarajia kuanza hivi karibuni mwezi Julai.


Jokate amempongeza Rais Samia kwa kugharamia matibabu ya Kijana Sativa aliyetekwa na watu wasiojulikana na kupatikana nje kidogo ya Pori la Hifadhi ya Katavi


Kampeni hiyo ya Kitaifa inatarajia kuzinduliwa Julai 6 katika Uwanja wa Banjamin Mkapa.


 

Post a Comment

0 Comments