Na Mwandishi Wetu,
DAR ES SALAAM.
Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Patrobas Katambi ameushukuru Ufalme wa Eswatini kuja Tanzania kujifunza mambo mazuri yaliyofanywa na Serikali kupitia Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) ambao umekuwa na ustahimilivu wa muda mrefu na unaweza kulipa mafao kwa wanachama wake. Mhe. Katambi amesema hayo Julai 18 , Jijini Dar es Salaam katika ofisi za NSSF wakati akizungumza na ujumbe kutoka Ufalme wa Eswatini ukiongozwa na Mhe. Mabulala Maseko, Waziri wa Utumishi wa Umma, Wabunge na wataalumu kutoka Mfuko wa PSPF wa nchini humo.
Katambi amesema baada ya kazi kubwa iliyofanywa na Serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi wa Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, NSSF imepata mafanikio mbalimbali yakiwemo kuwa na ustahimilivu wa muda mrefu na kuwa na uwezo wa kulipa mafao bila ya kutetereka kwa kipindi cha miaka 41 ijayo, na kuongeza kuwa NSSF imefanikiwa kuendesha shughuli zake kidijitali ambapo sasa wanachama wanaweza kupata taarifa zao mbalimbali kupitia simu ya kiganjani bila ya kulazimika kufika katika ofisi za NSSF.
Mhe. Patrobas Katambi, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu |
Kwa upande wake Waziri wa Utumishi wa Umma, Mhe. Mabulala Maseko amesema wamefurahishwa na hatua mbalimbali ambazo NSSF imepitia tangu kuanzishwa kwake na jinsi inavyofanya vizuri kwenye utendaji,mifumo ya TEHAMA na uwekezaji wake na kwamba wamekuja kujifunza kwa NSSF na kuona jinsi wanavyoendesha Mfuko ambao bado ni endelevu kwa kutoa huduma kwa wanachama. Hivyo Mifuko ya Hifadhi ya Jamii imekuwa na manufaa makubwa kwa kupunguza umasikini kwa wananchi, kuleta ustawi wa nchi na ukuaji wa uchumi ambapo inawaweka wananchi katika hali ya usalama kwa kuwa wana uhakika wa kufanya shughuli za maendeleo.
Huku Mwenyekiti wa Bodi wa Mfuko wa PSPF wa Eswatini, Bw. Sammy Dlamini, akisema wamejifunza mambo mengi mazuri yaliyofanywa na NSSF tokea ilipoanzishwa mpaka ilipofikia sasa.
Mabulala Maseko, Waziri wa Utumishi wa Umma – Eswatini |
Masha John Mshomba: Mkurugenzi Mkuu mpya wa NSSF |
0 Comments