Na AMEDEUS SOMI,
DAR ES SALAAM.
Naibu Mwenezi wa Chama cha ACT Wazalendo Shangwe Ayo amesema alichokifanya Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Nape Nnauye kuhusu chama chake kuwa kuna kushinda kwa aina nyingi licha ya Waziri huyo leo kujitokeza na kuomba msamaha anasema wao kama chama cha siasa wameshikilia jambo hilo kwa umuhimu mkubwa wakisema msamaha wake alioomba ni hadaa tu.
“Jana kwenye Mtandao wa x twitter zamani ameandika kwamba ni wapotoshaji wamekata clip tukasubiri atuwekee hiyo clip nzima ili awaoneshe wakosoaji wamekosoa hakuweka kwahiyo maana yake ni kwamba anamaanisha anachokiongea na imetushangaza sana kumuona Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye amempa haya madaraka hajakemea hiki kitendo wala kumuwajibisha, hatujaona kwake tu wiki iliyopita Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam aliwatukana wamachinga pale Simu 2000 Rais akakaa kimya, tunamuona Jerry Silaa kwenye mikutano yake ya utatuzi wa ardhi badala ya kutatua kero za migogoro ya ardhi anajifanya yeye ni mahakama ya ardhi na anatukana watanzania aliyewapa madaraka amekaa kimya ni wakati wa ACT Wazalendo kurudi chini kwa wananchi kuwaambia hiki chama hakiwafai kwa sababu hata aliyewapa madaraka anaona ni sawa watanzania kutukanwa”
Mbali na hayo Ayo ametangaza chama hicho kuanza ziara nchi nzima ambapo kwa kuanzia kiongozi mkuu wa Chama hicho Doroth Semu ataanza katika mikoa ya kanda ya Kati kuelekea Kaskazini.
Kwa upande wa Katibu Mkuu
wa Chama hicho Addo Shaibu atakwenda katika mikoa ya Kanda ya Ziwa, Isiaka
Mchinjita Makamu Mwenyekiti wa ACT atakwenda katika mikoa ya Kusini mwa
Tanzania na Mkoa wa Tanga.
Shangwe Ayo amesema Mwenyekiti mstaafu Zitto Kabwe atakwenda katika mikoa ya Kaskazini Magharibi pamoja na Mkoa wa Shinyanga
Lengo la ziara hiyo ni kuwaandaa wananchi kwenye kufanya uchaguzi wa Serikali za mitaa pamoja na kusajili wanachama million 10 kuelekea katika uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu na kusikiliza kero za wananchi wa mikoa hiyo.
Mwenyekiti wa ACT WAZALENDO Doroth Semu |
0 Comments