Na AMEDEUS SOMI,
DAR ES SALAAM
Mkurugenzi wa Shirika la Reli Tanzania Masanja Kadogosa amesema ujio wa Reli ya kisasa ya SGR haijaja kuchukua nafasi ya mabasi wala ndege kwani kuna watu wanaotaka kwenda na vyombo mbalimbali wanavyotaka wao.
Uzinduzi wa Kampeni ya SGR Umezinduliwa leo hii ambapo safari rasmi za Treni hiyo ya kisasa ya umeme zinatarajia kuanza siku ya Ijumaa Juni 14, 2024 kutoka Jijini Dar es Salaam hadi Morogoro.
“Reli hii haijaja kuchukua nafasi ya mabasi yaani hatujaja kushindana kwa sababu mabasi lazima yaendelee kuna watu wanafanya biashara kuna watu kule wameajiriwa serikali inapata kodi, mabasi lazima yaendelee, haijaja kuchukua nafasi ya ndege na watu wa ndege watakuwepo tu hao anataka yeye kutumia saa 1;15 au saa 1;30 yupo dodoma, kuna watu wanaotaka kwenda na treni ya haraka kuna watu ambao wanataka waende na malori, kuna watu ambao wanataka kwenda na mabasi hiyo ndio maana ya maendeleo watu wanataka kua na choice pana wanapotaka kufanya maamuzi ya kusafiri” amesema Kadogosa
Aidha Bwana Masanja amesema Treni hiyo katika kutoa huduma bora zaidi ya kushawishi umma kutakua na huduma za umeme wa kuchaji vifaa kama simu na pia huduma ya mtandao wa internet.
Mkurugenzi wa Shirika la Reli Tanzania Masanja Kadogosa akiwaonesha Waandishi wa habari mandhari ya ndani ya Treni ya SGR |
Nauli za usafiri huo itakua ni Shilingi elfu kumi na tatu 13.000 kwa daraja la kawaida kutoka Dar es Salaam hadi Morogoro na kwa awamu ya pili inayotarajia kuanza Julai 25 itakua shilingi elfu kumi na tano, 15.000 kwa daraja la kawaida na 18500 kutoka Dar hadi Makutupora.
Kwa upande wa zile za mchongoko bei kwa daraja la juu (Bussiness Class) itakua ni kati ya Shilingi laki moja hadi laki moja na elfu ishirini 100,000-120000 kutoka Dar hadi Dodoma.
0 Comments