HEADLINES

6/recent/ticker-posts

WIZARA YA KILIMO YAHITIMISHA KWA BAJETI YA TRILLIONI 1.24


 Na Mwandishi Wetu,

DODOMA.

Wizara ya Kilimo imehitimisha bajeti yake kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025 Bungeni jijini Dodoma kwa kishindo kikubwa.

Bajeti hiyo ya zaidi ya shilingi Trilioni 1.24 inatajwa kubeba matumaini ya mamilioni ya wakulima na watanzania wote kwa ujumla

Akiwasilisha bajeti hiyo, Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe (Mb) amesema malengo ya Serikali ni kuleta mageuzi katika Sekta ya Kilimo kwa kukifanya kilimo kuwa na tija zaidi katika uzalishaji wa mazao na kupanua wigo wa ajira zenye staha pamoja na utafutaji wa masoko.

Wizara ya Kilimo imelenga kutengeneza mazingira ya wakulima kuzalisha zaidi chakula cha kutosha nchini na kulisha wengine kibiashara, hivyo Wakulima wamehimizwa kubadilika na kuishi katika falsafa hiyo.


Post a Comment

0 Comments