Na MwandishiWetu,
DODOMA.
Serikali imefanikiwa kusajili wanafunzi 22,131 wakiwemo wasichana 2,794 wa elimu ya sekondari kwa njia mbadala katika vituo vya elimu ya watu Wazima pamoja na kutoa mafunzo ya kisomo kuimarisha stadi za Kusoma, kuandika na Kuhesabu kwa watu wazima 6,238 katika mikoa 26.
Aidha imeongeza idadi ya vituo vya elimu ya sekondari kwa njia mbadala kutoka 168 hadi kufikia 190 kwa lengo la kuongeza fursa kwa wanafunzi waliokosa elimu kwa sababu mbalimbali.
0 Comments