Na Mwandishi Wetu,
DODOMA.
Serikali imefanikiwa kusajili wanafunzi 22,131 wakiwemo
wasichana 2,794 wa elimu ya sekondari kwa njia mbadala katika vituo vya elimu
ya watu Wazima pamoja na kutoa mafunzo ya kisomo kuimarisha stadi za Kusoma,
kuandika na Kuhesabu kwa watu wazima 6,238 katika mikoa 26.
Hayo yamebainishwa na Waziri wa Elimu, Sayansi na
Teknolojia, Prof Adolf Mkenda alipokuwa akiwasilisha makadirio ya mapato na
matumizi ya fedha ya wizara hiyo kwa mwaka 2024/25ambapo amesema kuwa Serikali
imekamilisha moduli 11 za hatua ya I na ll kwa ajili ya vituo 151 vya elimu ya
sekondari kwa njia mbadala ili kuimarisha ufundishaji na ujifunzaji katika
vituo hivyo.
Aidha imeongeza idadi
ya vituo vya elimu ya sekondari kwa njia mbadala kutoka 168 hadi kufikia 190
kwa lengo la kuongeza fursa kwa wanafunzi waliokosa elimu kwa
sababu mbalimbali.
0 Comments