HEADLINES

6/recent/ticker-posts

MWELI: JIKITENI KWENYE UWAJIBIKAJI NA TEKNOLOJIA KUENDELEZA KILIMO


 Na Mwandishi Wetu,

DODOMA.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Bw.Gerald Mweli amesisitizia suala la Uwajibikaji wenye tija katika utekelezaji wa majukumu kwa Taasisi, Sekta Binafsi na Idara za Wizara ya Kilimo katika kuwahudumia wakulima na wanufaika katika mnyororo wa thamani kwenye kilimo.

Mweli ametoa rai hiyo wakati alipotembelea Maonesho ya Kilimo yanayoendelea katika Viwanja vya Bunge Jijini Dodoma. Maonesho yenye kali mbiu ya "From Lab to Farm."

Mweli aliingia katika eneo la maonesho hayo mchana kisha kuanza kutembelea mabanda ya wadau mbalimbali wa kilimo wanaotangaza shughuli zao zinazoakisi matumizi ya teknolojia katika utendaji wa shughuli za kilimo.

Mweli alisikika akitoa ushauri kwa wadau hao wa kilimo akiwataka kujikita zaidi katika uwajibikaji pamoja na kutumia zaidi teknolojia zinazotakiwa katika kuendeleza kilimo.

Akiwa katika banda la kampuni ya mbolea TFC aliwataka kuendelea kuhudumia wakulima kwa kuwafikishia bidhaa hiyo kwa wakati huku akiwa katika banda la TPHPA aliwapongeza na kuwataka kuendelea na harakati zao za kukabiliana na wadudu waharibifu wa mazao.

Akiwa kwenye banda la Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko( CPB), alipatiwa maelekezo kutoka kwa Meneja Masoko wa Bodi hiyo, Diana Fatukubonye ambaye alimwelezea Katibu Mkuu namna ambavyo CPB inatanua wigo wa shughuli zake za uuzaji wa mazao nchini.

Akiwa katika Banda la wadau wa Ushirika, Katibu Mkuu Mweli pamoja na mambo mengine alijionea namna mzani wa kidigitali unavyofanya kazi ikiwa pamoja na kupata maelezo kuhusiana na Benki ya Ushirika Kilimanjaro( KCBL)

Post a Comment

0 Comments