Na AMEDEUS SOMI,
DAR ES SALAAM.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt.Samia
Suluhu Hassan leo katika uzinduzi wa mkakati
wa Taifa wa matumizi ya Nishati safi ya kupikia ya mwaka 2024-2034 amesema kuwa Tarehe 14 Mei mwaka huu Tanzania
itakua Mwenyekiti mwenza katika Mkutano wa nishati safi ya kupikia barani
Afrika utakaofanyika Jijini Paris
Ufaransa na unatarajia kuhudhuriwa na watu 900wakiwemo wakuu wa nchi na
Serikali, Taasisi za kifedha, Washirika
wa Maendeleo, Wanazuoni, Watekelezaji wa Nishati Jadidifu, Wadau wa sekta
binafsi nk.
Masuala muhimu yatakayojadiliwa ni pamoja na ufadhili wa miradi ya nishati safi ya kupikia na masuala ya kisera na ushirikiano katika kusukuma ajenda ya nishati safi ya kupikia ambapo Rais Samia amesema katika Mkutano huo.
“Bara la Afrika tunakwenda kupaza sauti kwa mashirika ya fedha na wadau wao wanaowachangia kwenye mashirika ya fedha kupitia mizunguko mbalimbali wanayochanisha fedha kwa mfano kwa upande wa benki ya Dunia wana mzunguko wanaita IDA wana watu wao, wajumbe wao wanaowachangia benki ya Dunia tunakwenda kuwaomba waongeze michango wasirudi nyuma ili Afrika iendelee kuwa bara litakalotoa huduma ya bure kwa Ulimwengu kunyonya hewa ya Carbon kwenye misitu yetu lazima watuwezeshe tuelekee kwenye nishati safi ya kupikia”
Aidha Rais Dkt.Samia ameendelea kusema kuwa kuna majadiliano watakwenda nayo ya kuwa watu waache kutumia gesi lakini watumie gesi “Sisi Afrika tunakwenda kupaza sauti watuwezeshe tuendelee kutumia gesi kuelekea kwenye matumizi ya nishati nyingine tutakazokua tunajadiliana kila tunavyokwenda lakini kwa sasa Mungu ametubariki na gesi lazima watuwezeshe kutumia gesi ili tuipe nafuu sekta ya misitu ipumue na iweze kutoa huduma ya bure kwa Ulimwengu kuweza kunyonya hewa ukaa inayotoka n ahii hewa ukaa sisi tunatoa asilimia tano tu lakini nyingi inatoka huko kwao sisi tunawanyonyea huku, kwahiyo ili Afrika iendelee kuwa shamba lao basi watuchangie tuweke miundombinu na tuweke utaratibu wa kuweka nishati safi ya kupikia ili miti ipumue”
Rais Samia amesema kufikia asilimia 80 ya matumizi ya nishati safi ndani ya kipindi cha miaka 10 haitakuwa kazi rahisi lakini penye nia pana njia hivyo kwa kuwa wote tuna nia moja tutafikia azma ya malengo yetu kwa kila mdau atatumia kipawa na maarifa yake basi tutafika iyo 2034.
Vilevile Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan ametoa agizo kwa Wizara
ya Nishati kuhakikisha inawafikishia wadau mkatati huu kwa njia rasmi na pia iuweke
katika Tovuti na mitandao ya kijamii ya
wizara kwa lugha za Kiswahili na Kiingereza.
Agizo la pili alilowapa Wizara hiyo ni kukaa na wadau husika
wa Serikalini na Sekta binafsi kubaini maeneo ambayo yakifanyiwa kazi
yataongeza uharaka wa matumizi ya nishati safi ya kupikia kwa bei nafuu ili
wananchi wengi zaidi waweze kutumia akihimiz kushirikiana na sekta za fedha na
mipango kufanikisha hilo.
Agizo la tatu ni kuwa na mfuko wa nishati safi ya kupikia ifikapo
mwaka 2025 akiwaagiza kuja na sheria itakayowezesha kupatikana kwa mfuko huu, la
nne ni TAMISEMI iboreshe mikataba wanayoingia na Wakuu wa Mikoa na Wilaya ili
kuongeza kifungu cha matumizi ya nishati safi ya kupikia kwenye upimaji wa
utendji kazi wao.
0 Comments