HEADLINES

6/recent/ticker-posts

HIVI HAPA VIPAUMBELE VITANO SEKTA YA ELIMU MWAKA WA FEDHA 2024-25


Na Mwandishi Wetu,
DODOMA.

Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Imetaja vipaumbele vitano muhimu katika sekta ya Elimu nchini kwa mwaka wa fedha 2024-25 ambao Waziri wa Wizara hiyo @professoradolfmkenda ameviweka bayana bungeni muda huu wakati anawasilisha bajeti ya Wizara hiyo Jijini Dodoma.

“Vipaumbele vya Wizara Elimu kwa mwaka wa fedha 2024/25 ni kama vifuatavyo:

Kuendelea na utekelezaji wa sera na mitaala, mapitio ya sheria na kuandaa miongozo ya utoaji elimu na mafunzo nchini

Kuongeza fursa na kuimarisha ubora wa elimu ya ufundi na mafunzo ya ufundi stadi (amali na amali sanifu);

Kuongeza fursa na kuimarisha ubora wa elimu ya msingi, sekondari na ualimu;

Kuongeza fursa na kuimarisha ubora wa elimu ya juu; na kuendeleza tafiti, matumizi ya sayansi, teknolojia na ubunifu.

Kuendelea na utekelezaji wa Sera na Mitaala, Mapitio ya Sheria na kuandaa Miongozo ya Utoaji Elimu na Mafunzo Nchini“ - Prof Adolf Mkenda waziri wa Elimu Sayansi na teknolojia @wizara_elimutanzania


Post a Comment

0 Comments