LAGOS NIGERIA.
Vita ya ndoa kati ya mshambuliaji wa Nigeria, Olarenwaju Ayobami(31)
Kayode wa Klabu ya Gaziantep FK inayoshiriki Ligi Kuu Nchini Uturuki ya Super
Lig ameingia katika mtafaruku mkubwa na mkewe Bi Ezinne Kayode ambaye kwa sasa
wameachana kutokana na majibu ya vipimo vya DNA kufichua kuwa Watoto wa Bi
Ezzine sio wa mchezaji Kayode.
Baada ya sekeseke la muda bwana Kayode aliamua kufata hatua
za kisheria kuhusu suala hili ambapo mkewe alimgeuzia kibao na kusema kwamba Kayode
alitoa taarifa hizi na kusababisha kusambaa katika mitandao ya kijamii juu ya
taarifa ya majibu ya DNA ambayo yalisema
kuwa Watoto watatu Jason. , Jayden na Jamin,sio wa mchezaji Olarenwaju Kayode SUNDAY PUNCH liliripoti.
Ezinne anasema alikasirika baada ya madai hayo kutolewa na bwana Kayode na mara moja anamtaka akanushe baada ya kusambaa kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii Jumamosi.
Ukweli daima utakuwa daima; njama yako na timu yako ya PR
kubadilisha masimulizi kwa ujanja ilifunuliwa kwangu kabla ya hapo. Kwa wakati
ufaao, ulimwengu utajua ni maovu kiasi gani uliyofanya kwa taasisi ya ndoa na
kuunda hadithi karibu na DNA kama mlivyopanga yote haitaokoa siku kwa ajili
yenu.
0 Comments