HEADLINES

6/recent/ticker-posts

ULEGA AKABIDHI CHAKULA, BOTI KWA WAATHIRIKA WA MAFURIKO RUFIJI


Na Mwandishi Wetu,
RUFIJI.

Waziri wa Mifugo na Uvuvi, ambaye pia ni Mbunge wa Mkuranga,  Abdallah Ulega amefika Wilayani Rufiji, mkoani Pwani kuwafariji waathirika wa mafuriko na amekabidhi tani 4 za chakula na boti pamoja na mashine yake ili viwasaidie waathirika hao.

Ulega amekabidhi vitu hivyo leo Aprili 11, 2024 kwa Mbunge wa Rufiji ambaye pia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI, Mohamed Mchengerwa kwa niaba ya wananchi wa Rufiji waliopatwa na mafuriko.

Aidha, Wakati akikabidhi vitu hivyo Waziri Ulega ametoa pole kwa waathirika wote wa mafuriko huku akitoa shukrani kwa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa anayoifanya ya kuhakikisha wananchi hao wanapata kila kinachostahili ili waweze kuendelea na maisha yao ya kawaida.



Post a Comment

0 Comments