Na Mwandishi Wetu,
DODOMA.
Waziri wa TAMISEMI, Mohamed Mchengerwa amesema katika mwaka 2024/25, TAMISEMI imepanga kutumia shilingi bilioni 190.57 kwa ajili ya ununuzi wa magari ya Viongozi wa Mikoa na Wilaya, kuendelea na ujenzi, ukarabati na ukamilishaji wa miundombinu ya Mikoa ikiwemo majengo ya utawala, Ikulu ndogo, makazi ya Viongozi na Watumshi wa Mikoa, Wilaya na Tarafa katika Mikoa 26. Mchengerwa ametoa taarifa hiyo Bungeni Jijini Dodoma leo April 16,2024 wakati akitoa hotuba kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka 2024/2025 ambapo amesema shughuli zitakazotekelezwa katika utawala bora ni pamoja na ununuzi wa magari 9 ya Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala wa Mikoa katika Mikoa ya Katavi, Njombe, Iringa, Kigoma, Mwanza, Singida, Dar es Salaam na Manyara” “Shughuli nyingine ni ununuzi wa magari 56 ya Wakuu wa Wilaya na 47 ya Wakurugenzi wa Halmashauri”
0 Comments