HEADLINES

6/recent/ticker-posts

SERIKALI IMEANZISHA SHAHADA ZITAKAZOSAIDIA KUBORESHA HUDUMA ZA UTENGAMAO


Na Mwandishi Wetu,
DAR ES SALAAM.

Serikali kupitia Wizara ya Afya ikishirikiana na Chuo Kikuu cha Muhimbili (MUHAS) imeanzisha Shahada ya kwanza ya Sayansi ya Mazoezi Tiba ya kusaidia mawasiliano (Speech pathology), Tiba Kazi (Occupational therapy) na Tiba Viungo (Physiotherapy) kuanzia mwaka 2023/24 ili huduma za utengamao zipewe kipaumbele. 

Waziri wa Afya Mhe. Ummy Muwalimu amesema hayo leo Aprili 28, 2024 banda ya mbio za ‘Run4Autism’ (watoto wenye Usonji) za KM 5 zilizoanzia katika viwanja vya farasi kupitia daraja la Tanzanite Jijini Dar Es Salaam zikiongozwa na mgeni rasmi Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa. 
“Pia, tutaanzisha na shahada ya kwanza ya Sayansi ya Saikolojia ya Tiba (Clinical Psychology) kuanzia mwaka 2024/25 lengo kubwa la kuanzisha shahada hizi ni kuhakikisha huduma za utengemao zinapewa kipaumbele cha juu na Serikali chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, huduma za magongwa Yasiyoambukizwa pamoja na huduma za Afya ya Akili”. Amesema Waziri Ummy 

Amesema, Serikali inaendelea kufanya juhudi za kutatua changamoto za watu wenye Usonji ambapo amebainisha miongoni mwa changamoto hizo hi pamoja na upungufu wa wataalam wa mazoezi tiba pamoja na gharama za mazoezi tiba kwa watu wenye Usonji.

“Tunategemea pia kuanzisha fani hizi katika ngazi Diploma kwa Mwaka wa fedha 2024/25 ili tuweze kuwa na watalaam wengi zaidi wa masuala ya ‘Speech pathology’, ‘Occupational therapy’, ‘Physiotherapy’ katika ngazi za vituo vya Afya na Hospitali za Wilaya nchi nzima. 

Kwa upande wake Mwanzilishi na Mkurugenzi Mtendaji wa Lukiza Autism Tanzania Bi. Hilda Nkabe ameishukuru Serikali kupitia Wizara ya Afya kwa kuona umuhimu wa kuanzisha Shahada hizo kwa lengo la kuelimisha na kuwatambua watu wenye Usonji. 

“Tunashukuru sana Serikali kwa kutuunga Mkono kwenye Taasisi yetu pamoja na kutambua watu wenye Usonji, tunaomba Serikali iendelee kuwapa kipaumbele hasa kwenye elimu pamoja na kazi za ufundi ambazo pia zinaweza kufanywa na watu wenye Usonji.” Amesema Waziri Ummy

Post a Comment

0 Comments