Na AMEDEUS SOMI,
DAR ES SALAAM.
Mkurugenzi wa Nsong’wa Traditional Clinic, Dkt Damaki amesema ipo haja ya kujali afya za jamii pasipo kubagua wala kuchagua rika au makundi ya watu ndio maana wameamua kutoa misaada ya kiafya itakayowasaidia Watoto kujilinda katika changamoto mbalimbali za maradhi.
Dkt. Damaki ameyasema hayo Leo Aprili 17, 2024 wakati akitoa msaada kwa watoto yatima wanaoishi katika mazingira magumu katika Kituo cha Faraja Orphanage kilichopo Mburahati, Dar es Salaam.
Akipokea msaada huo Bi Zamda Juma ambaye ni msimamizi kituoni hapo ametoa shukrani kwa Taasisi ya Nsong'wa Tradition Clinic kwa msaada huo huku akitoa rai kwa wadau wengine kuwasaidia kupata bima za afya ambazo ni changamoto kwa watoto wanaoishi kituoni hapo.
"Tunashukuru sana kama Faraja kwa msaada huu, lakini bado tunachangamoto za bima za afya kwahiyo atakaye jaaliwa anaweza kutusaidia" amesema Zamda ambaye ni mlezi katika kituo hicho.
0 Comments