Na Mwandishi Wetu,
Waziri wa Kilimo, Mhe. Husein Bashe amezitaka Taasisi na Kampuni binafsi zinazojihusisha na kilimo kujikita zaidi katika ubunifu na matumizi ya Teknolojia ili kuongeza tija na ufanisi kwenye sekta hiyo.
Waziri Bashe ametoa ushauri huo leo April 30, 2024 wakati alipotembelea kukagua mabanda ya wadau mbalimbali wa kilimo wanaoshiriki maonesho ya kilimo ya siku tano yanayoendelea kwenye viwanja vya Bunge Jijini Dodoma.
Akiwa katika Maonesho hayo yenye Kauli mbiu ya "From Lab to Farm" Waziri Bashe amepata wasaha wa kujionea namna teknolojia na ubunifu unavyochangia maendeleo ya sekta ya kilimo.
Baadhi ya Wageni mbalimbali wakiwemo wabunge wametembelea maonesho hayo.
0 Comments