HEADLINES

6/recent/ticker-posts

WATANZANIA WAPEWA MBINU ZA KUJIKINGA NA MAGONJWA YA KINYWA NA MENO

Na AMEDEUS SOMI
DAR ES SALAAM,

Wataalamu wa Afya ya Kinywa wanashauri Mtu ambaye hana changamoto za Kinywa kama kuumwa Jino, Fizi kuvimba au kutoa Damu kuwa na utaratibu wa kufanya uchunguzi wa kinywa angalau mara 2 kwa Mwaka katika Vituo vyenye Wataalamu waliothibitishwa.

Hata hivyo, kwa wale wenye changamoto za Kinywa wanashauriwa kuwaona Wataalamu wa Afya ya Meno na Kinywa mara kwa mara kwa ushauri na tiba ya Changamoto zao.

Ni katika maadhimisho ya afya ya akinywa na meno Duniani ambayo huadhimishwa kila ifikapo tarehe 20 mwezi machi ya kila mwaka ambapo Kaimu Mkuu wa Chuo cha Muhas Profesa Emmanuel Bulandya ameeleza hayo.


Hata hivyo kwa upande wa Mkuu wa Chuo cha Kinywa na Meno Dkt.Matilda Mtaya amesema hii hali ya watu wengi kupenda kuwekewa Senyenge au waya maalum kwenye meno sio fasheni bali senyenge hizo huwekwa kitaalamu na lengo kubwa ni kwa ajili ya kurekebisha mpangilio wa meno.

Akitaja sababu zinazopelekea mpangilio mbaya wa meno ikiwemo ajali zinazoweza kuharibu taya hivyo mpangilio wa meno kuvurugika, sababu za kurithi, mtoto kupoteza meno wakati wa ukuaji, ulaji wa vyakula vyenye sukari na mtoto kunyonya vidole.

Kaulimbiu ya siku hiyo ni Kinywa cha furaha ni mwili wa furaha.

Post a Comment

0 Comments