HEADLINES

6/recent/ticker-posts

RAIS MWINYI ASHUKURU WATANZANIA KUTOA USHIRIKIANO MSIBA WA BABA YAKE



 Na Mwandishi Wetu,

DAR ES SALAAM.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi amesema familia ya Marehemu Mzee Ali Hassan Mwinyi imepata faraja kubwa kutokana na Dua Maalum zilizofanywa Bara, Visiwani na nje ya nchi katika Misikiti mbalimbali kwa ajili ya kumuombea Hayati Mzee Mwinyi. 

Rais Dk.Mwinyi amesema hayo alipojumuika na Waumini wa Dini ya Kiislamu katika ibada ya Sala ya Ijumaa na Dua Maalum ya kumwombea  Hayati Alhajj Mzee Ali Hassan Mwinyi Misikiti wa Al Jumaa Masjid Kitumbini Dar es Salaam tarehe: 22 Machi 2024.

Aidha Rais Dk.Mwinyi ameushukuru uongozi wa Msikiti wa Al Jumaa Kitumbini kwa kuandaa Dua Maalum ya kuombea Hayati Mzee Ali Hassan Mwinyi.

Post a Comment

0 Comments