Na Mwandishi Wetu,
DAR ES SALAAM.
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam kwa kushirikiana na kikosi kazi maalum cha
kuzuia na kupambana na matumizi ya makosa ya kimtandao kimeendelea na kazi ya ufuatiliaji na
kufanikiwa kwa mara nyingine kuwakamata Claudian Makaranga (28) mkazi wa Kawe, Kinondoni
na Hongliang Yang (35) Mchina, mkazi wa Kigamboni, kwa tuhuma za kuingiza vifaa vya
mawasiliano ya intanet nchini bila kufuata utaratibu wa kisheria vyenye jina la STARLINK
KIT/DEVICE.
Watuhumiwa hao wamekuwa wakijitangaza kuuza vifaa na kutoa huduma ya internet nchini kupitia
mtandao ya kijamii wa Instagram kwa akaunti yenye jina la STARLINK.
Baadhi ya vifaa vilivyoingizwa nchini imebaika vilishauzwa na kutumika katika baadhi ya maeneo
ya Dar es Salaam kitendo ambacho ni kosa na kinyume na sheria kwani havijaidhinishwa na
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA).
Vifaa vilivyokamatwa ni Starline Dish 12, Starlink
Router 12.
Polisi Kanda Maalum ya Dar inatoa wito kwa wananchi kuwa makini na matumizi ya vifaa vya
mawasiliano, ambavyo havijaidhinishwa na mamlaka husika.
Pia amekamatwa Wilfred Werandumi (44) mkazi wa Tungi, Morogoro na Abdulrahim Mwakibinga
(30), Mkazi wa Mwandege, Morogoro kwa tuhuma za kutumia majina ya Viongozi mbalimbali wa
nchi kutapeli watu, kwa kujifanya wanaomba michango ya harusi, misiba na matibabu.
Baadhi viongozi ambao majina yao yametumika katika utapeli huu ni Mh. Dr. Stergomena Tax,
Mhe. Innocent Bashungwa, Mhe. Mohamed Nchengerwa, Mhe. Eng. Hamadi Masauni, na Katibu
Mkuu wa zamani wa CCM Daniel Chongolo.
Amekamatwa pia Salum Kingu (25) mkazi wa Mbalizi, Mbeya na Loveness Silonga (24) mkazi wa
Mbalizi, Mbeya kwa tuhuma za kutumia akaunti ya mtandao wa kijamii wa Facebook yenye jina la
KOPA FASTER TULIA TRUST FOUNDATION na kujipatia pesa kwa njia ya udanganyifu kutoka
Ofisiya: -
Kamanda wa Polisi,
Kanda Maalum,
S.L.P.9140,
DAR ES SALAAM
……………
Simu: +255 (0) 22-2117705
Nukushi: +255(0) 22-2121 524
Baruapepe:
utawala.dsmz@tpf.go.tz
23/01/2017
33
kwa watu mbalimbali kwa kudai kuwa wanatoa mikopo kwa masharti nafuu na haraka wakitumia
namba ya simu 0749704445.
Jeshi la Polisi linaendelea na ufuatiliaji mkali wa tabia hizi na watuhumiwa wote watashughulikiwa
vikali kwa mujibu wa sheria.
Imetolewa na ;
Muliro J. MULIRO - SACP
Kamanda wa Polisi
Kanda Maalum ya Dar es Salaam
0 Comments