HEADLINES

6/recent/ticker-posts

KAMATI YA BUNGE YAZURU TSHTDA YARIDHISWA UJENZI GHALA LA CHAI

Na Mwandishi Wetu,
DAR ES SALAAM.

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara, Kilimo na Mifugo akiambatana na Waheshimiwa wajumbe wa Kamati leo tarehe 18 Machi, 2024 katika ziara yao ya ukaguzi wa miradi ya Serikali wamekagua ujenzi wa ghala la Kipawa Dar es Salaam katika Taasisi ya Wakala wa Wakulima Wadogo wa Chai Tanzania (TSHTDA) ambalo ujenzi wake umegharimu Shilingi 743,854,516 ikiwa ni gharama ya mkandarasi na mshauri elekezi. 

Lengo la ghala hili ni kuimarisha uwezo wa Taasisi katika kutekeleza majukumu yake pamoja na kuchangia kutoa ajira kwa umma wa watanzania kupitia wananchi watakaotumia ghala hilo.


Nao Uongozi wa TSHTDA ulitoa changamoto zao ambapo walisema changamoto  kubwa kwenye mradi huu ilikuwa ni ufinyu wa bajeti ambayo ingewezesha kutekeleza kazi zote ambazo zilikusudiwa katika mpango wa awali wa Mradi. 

Baada ya mambo mengine, Mwenyekiti na Wajumbe wameridhika na ujenzi unaoendelea na kusema ghala lipo vizuri na linapendeza. Aidha, waliuelekeza Uongozi wa TSHTDA urekebishe barabara ya kuingia ghalani kwa kuwa ghala hilo litatumika wakati wa  mnada ambao utakuwa wa kimataifa  na utahudhuriwa na watu mbalimbali. 

Ziara hii pia imehudhuriwa na Naibu Waziri wa Kilimo Mhe.David Silinde (Mb), Menejimenti ya Uongozi wa Wakala wa Wakulima Wadogo wa Chai Tanzania ikiongozwa na Mkurugenzi Mkuu Ndg. Theophord Cosmas Ndunguru, Mwakilishi kutoka Bodi ya Chai Tanzania, Mkandarasi Mwelekezi ambaye ni Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) pamoja na Mkandarasi wa Ujenzi kutoka kampuni ya HERA.




Post a Comment

0 Comments