Hii ni kutokana na ufuatiliaji maalum unaoendelea unaofanywa
na Jeshi la Polisi kwa kushirikiana kikosi kazi maalum cha kuzuia na kupambana
na makosa ya kimtandao. Waliokamatwa ni pamoja na Obadia Kwitega (35) mkazi wa
Kigamboni na Issa Mwamba (28) mkazi wa Tabata Segerea.
Wamekamatwa kwa tuhuma za kumiliki televisheni ya mtandaoni
ya kwenye Youtube iliyotambulika kwa jina la Jamii Digital, na akauti ya
mtandao wa X iitwayo SUKUNUNU 01, waliyokuwa wanazitumia kusambaza taarifa za
uongo na za uchochezi kuhusu viongozi wakuu wa Serikali. Baadhi ya taarifa zao
zilisomeka “MKAKATI WA SIRI JANUARY MAKAMBA KUMNG’OA RAIS SAMIA 2025”
Katika hatua nyingine
Jeshi la Polisi limemkamata pia Frank Mbetu (35) mkazi wa Ligula, Mtwara kwa
tuhuma za kujifanya mtumishi wa Serikali ngazi ya Katibu Mkuu Kiongozi na
kujipatia pesa kwa njia ya udanganyifu kuwa angewapa watu kazi serikalini au
kupandishwa vyeo.
Amekamatwa pia Honest Mgona (47) mkazi wa Mabwepande kwa
kujipatia pesa kwa njia ya udanganyifu kuwa ametumwa na Mhe. Mohamed Nchengerwa
(MB), Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za mitaa
kusambaza mitungi gesi kwa wananchi na baadae kuwatapeli kwa kuwadai pesa za
usafiri. Mwingine ni Edwin Kasebele@ Marlin (24) Mkazi wa Mapelele, Mbeya
anayetuhumiwa kusambaza taarifa za uongo kupitia mtandao wa kijamii wa Ofisiya:
- Kamanda wa Polisi, Kanda Maalum, S.L.P.9140, DAR ES SALAAM …………… Simu: +255
(0) 22-2117705 Nukushi: +255(0) 22-2121 524 Baruapepe: utawala.dsmz@tpf.go.tz
23/01/2017 33 2 ‘Facebook’ na ‘Whatsapp’ kuwa anafanya biashara ya vitenge na
hivyo kujipatia pesa kwa udanganyifu kutoka kwa watu mbalimbali.
Watuhumiwa hao wamekutwa wakiwa na simu 7 na kadi za za simu
13 za makampuni mbalimbali ya simu ambazo wamekuwa wakitumia kama nyenzo
kutekeleza uhalifu wao. Kutokana na vitendo hivi vya kihalifu kwa njia ya
mtandao, Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linatoa rai kwa wananchi
kuwa makini na matumizi ya mitandao na Jeshi la Polisi linaendelea kuwachukulia
hatua kali watu wengine wanaokiuka sheria, kanuni na taratibu za matumizi
sahihi ya mitandao.
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linawahimiza
wananchi kuendelea kutoa taarifa kwenye kituo cha Polisi kilicho karibu ili
hatua stahiki zichukuliwe haraka. Jeshi la Polisi pia linawahimiza wananchi
kuendelea kutotoa CV, namba ya NIDA au vitambulisho, nywila (password) au namba
ya siri (PIN) kwa mtu yeyote bila kuwa na uhakika na kinachofanyika. Katika
hatua nyingine, Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linachunguza
tukio la kuuwawa kwa mtoto wa miaka 7 mwanafunzi wa shule ya msingi Kibonde
maji B, Mbagala na mwili wake kukutwa tarehe 13 Machi, 2024 kwenye msitu wa
Jeshi karibu na Shule aliyikuwa anasoma.
Mtoto huyo aliondoka
nyumbani kwao na mtoto mwenzake tarehe 12 Machi 2024 majira ya 11:30 jioni.
Mwili wa marehemu umehifadhiwa Hospitali ya Polisi Kilwa road kwa uchunguzi
zaidi. Ufuatiliaji mkali unaendelea kumtafuta mtuhumiwa/ watuhumiwa waliohusika
ili hatua kali za kisheria zichukuliwe dhidi yao.
Imetolewa na Muliro J. MULIRO - SACP Kamanda wa Polisi Kanda
Maalum ya Dar es Salaam
0 Comments