Na Amedeus Somi,
DAR ES SALAAM,
Daktari aliyegundua dawa za tiba asili zinazotibu magonjwa
sugu mbalimbali kama UTI,Saratani na ukosefu wa nguvu za kiume ametaja sababu
zinazopelekea usugu na namna bora ya kutatua matatizo ya magonjwa hayo.
Akizungumza Jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa ofisi mpya za utoaji wa
huduma za dawa hizo zilizopo DDC Mlimani City Daktari bingwa wa tiba asili
kutoka katika Kliniki ya Nson’gwa Herbal Kliniki Dkt. Damaki ametaja sababu zinazopelekea
usugu wa magonjwa hayo pamoja na njia bora za kutibu magonjwa hayo.
“Unapokaa na ugonjwa wa fangasi kwa muda mrefu ama UTI Inakua inajirudiarudia mara kwa mara wanajitibu kwa muda mfupi inajirudia na wakati mwingine hawajui kuwa ugonjwa huu una madhara makubwa sana na bakteria hawa wa fangasi wanaingia kwenye mirija ya uzazi hivyo kupelekea ugonjwa wa PID hivyo kuleta athari ya kushindwa kupata ujauzito”
Katika hatua nyingine Dkt.Damaki amezungumzia janga la
ukosefu wa nguvu za kiume kwa vijana na watu wazima akisema kwamba kitendo cha
wanaume kushindwa kufika kileleni kunasababishwa na sababu kadhaa ikiwemo
vijana kujichua hivyo kupelekea mishipa kupata maambukizi.
Dkt.Damaki amesema migogoro mingi inayosababisha ndoa nyingi
kuvunjika ni kutokana na wanaume wengi kushindwa kumfikisha kileleni mwanamke akijinadi
dawa ya nkamba kumaliza tatizo la kushindwa kufika kileleni.
“Kuna wale ambao hawawezi kurudia katika mizunguko yao na kama ukishindwa kwenda zaidi ya dakika 30 au 25 katika safari moja bado ni changamoto kwahiyo kama una tatizo hilo fika ofisini kuchukua dawa na tumepeka punguzo katika kipindi hiki cha ufunguzi”
Nao mashuhuda waliopona kwa kutumia dawa za Kliniki hiyo wakasema namna ambavyo dawa za Daktari huyo zimeweza kuwasaidia.
“Nimeugua kwa muda mrefu sana tangu mwaka 2017, Nilikuwa naugua maradhi ya neva na viungo nilikwenda katika Hospitali nyingi sana lakini hakuna nafuu yoyote niliyoipata hivyo baada ya kusikia Nsong’wa Clinic niliwatafuta na kuwapata hivyo nilipokutana na Dkt.Damaki sukari ilianza kushuka na kuwa sawa baada ya kutumia dawa zake hali yote ilipotea na kwa sasa nipo safi kabisa”.
Amesema Jonas Kwayu Mkazi wa Dar es Salaam.
Kumekua na kawaida ya watu wengi kushindwa kuamini katika dawa za mitisha ba lakini kwa upande wa Daktari Damaki ameonesha ushuhuda kwa wengi na imebainika dawa zake zinatibu na kumaliza matatizo mengi ya kiafya.
Kliniki hiyo ambayo imezinduliwa leo, dawa zake zimesajiliwa
na Baraza la Tiba asili Tanzania pamoja na Mamlaka zote zinazohusiana na tiba nchini
kinapatikana DDC Mlimani City jijini Dar es Salaam na rasmi imeanza kutoa
huduma.
0 Comments