Na Mwandishi Wetu,
LINDI.
Waziri wa Afya Ummy Mwalimu amezitaka Halmashauri ikiwemo ya Wilaya ya Kilwa kuajiri watumishi wa mikataba kwa kutumia mapato ya ndani ili kupunguza changamoto za uhaba wa wataalamu wa Afya katika Wilaya hizo.
Waziri Ummy amesema hayo Februari 28, 2024 baada ya kupokea taarifa ya hali ya Afya katika Halmashauri ya Wilaya hiyo iliyotolewa na Mganga Mkuu wa Wilaya hiyo Dkt. Lusajo Mwakajoka ambayo inaonyesha hali ya upatikanaji wa huduma za Afya katika Mkoa wa Lindi, upatikanaji wa Vifaa na Vifaa Tiba pamoja na changamoto.
“Tutatumia njia kuu Tatu ili kupunguza changamoto za watumishi ikiwa ni pamoja na njia ya vibali vya ajira kutoka Ofisi ya Rais Utumishi, kuajiri watumishi kupitia mapato ya ndani ya Halmashauri pamoja na wadau wetu wa maendeleo katika Sekta ya Afya nao wanaajiri ajira za mikataba pamoja.” Amesema Waziri Ummy
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Lindi Zainab Telack amemshukuru Waziri wa Afya Ummy kwa kufanya ziara katika Mkoa huo na kumuomba aupe kipaumbele kwa kuwa una wananchi wengi wa kipato cha chini ambao hushidwa kufata huduma mbali na makazi yao.
Nyinginezo
WAZIRI MKUU JAMHURI YA KIDEMOKRASIA YA SHIRIKISHO LA ETHIOPIA KUWASILI NCHINI KWA ZIARA YA SIKU TATU
“Vifaa tiba ikiwemo Dawa zinaposambazwa na Bohari Kuu ya Dawa (MSD) tunaomba wawe wanawahi kwa wakati kwa kuwa wananchi wengi wa Mkoa wa Lindi wanakipato cha chini, dawa zinapochelewa tunamkwamisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwakuwa ameshatoa fedha za dawa, kikubwa ni sisi watendaji.” Amesema Telack
Waziri Ummy anaendelea na ziara yake katika Mkoa wa Lindi na anatarajia kutembelea na kukagua hali ya utoaji wa huduma katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Lindi (Sokoine), Hospitali za Wilaya, Vituo vya Afya pamoja na Zahanati.
Katika ziara hiyo Waziri Ummy ameambatana na timu kutoka Wizara ya Afya akiwemo Mkurugenzi Msaidizi wa Hospitali za Rufaa za Mikoa Dkt. Caroline Damian anaemuwakikisha Mkurugenzi wa huduma za Tiba, Mkurugenzi Msaidizi wa Rasilimali watu upande wa Hospitali za Rufaa za Mikoa Bw. Danny Temba
0 Comments