Na Mwandishi Wetu,
ARUSHA.
Hamasa
ya kujiandikisha na kuhama kwa hiari kutoka ndani ya Hifadhi ya Ngorongoro kwenda
katika Kijiji cha Msomera wilayani Handeni inazidi kupamba moto baada ya kundi
la 5 la awamu ya pili kuhama likiwa na kaya 67 zenye watu 592 na Mifugo 2,790.
Wananchi
hao waliokuwa wakiishi ndani ya Hifadhi ya Ngorongoro na kuamua kuhama kwa
hiyari wameagwa rasmi siku ya Alhamisi
01.02.2024 na Kamishina wa
Uhifadhi wa Mamlaka ya Hifadhi ya
Ngorongoro Bw.Richard Kiiza ambapo aliwaomba wenyeji wanaohama kutumia fursa
waliopata kuendelea kuwapa habari na kuwashawishi ndugu zao ambao bado
hawajajiandikisha ili waweze kujiandikisha na kuondokana na maisha duni wanayoishi
ndani ya Hifadhi.
Amesema
kuwa serikali kupitia Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro inaendelea na
uhamasishaji wa wananchi ambapo kwa sasa
mwamko wa watu wanaoishi ndani ya hifadhi kutaka kuondoka umeongezeka
huku akisisitiza kuwa serikali itaendelea kuheshimu haki zote za msingi za
wananchi hao.
Akitoa taarifa ya maendeleo ya zoezi hilo Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Mamlaka hiyo Bw. Fedes Mdala ambaye pia ni Meneja wa mradi huo amesema kuwa hadi kufikia sasa jumla ya kaya 934 zenye watu 5,747 na mifugo 26,227 zimeshaondoka ndani ya hifadhi.
Bw.Mdalla
amesema hatua mbalimbali za utekelezaji wa mradi huo zimeendelea kuchukuliwa na kuzitaja hatua hizo kuwa ni
ujenzi wa nyumba, uhamasishaji, Uandikishaji wa maendeleo yaliyofanywa ndani ya
Hifadhi na uhamishaji wa wanachi kwenda Msomera na maeneo mengine.
Kwa
upande wake Mwakilishi kutoka wizara ya Mailiasili na Utalii Bw. John Mapepele amewapongeza wananchi hao kwa kufanya uamuzi
sahihi ambao unakwenda kubadilisha maisha yao.
Serikali
kupitia wizara ya Maliasili na Utali,Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro pamoja na
wizara nyingine za kisekta zinaendelea na utekelezaji wa kuhamisha watu kutoka
ndani ya Hifadhi ili kuboresha maisha ya wananchi na kulinda hifadhi hiyo yenye
hadhi mahsusi duniani.
0 Comments