HEADLINES

6/recent/ticker-posts

WAGONJWA 40 KUBADILISHWA NYONGA MOI

 


Na Mwandishi Wetu,

DAR ES SALAAM.

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOI) Prof. Abel Makubi amewapokea madaktari bingwa  wabobezi wa upasuaji wa nyonga Watatu kutoka nchi ya Pakistan watakaoendesha kambi ya siku tano ya upasuaji wa nyonga kwa wagonjwa 40 kwa kushirikiana na madaktari bingwa wa MOI. 

Katika kambi hiyo iliyoanza jana  Februari, 26, 2024 jumla ya wagonjwa 40 wanatarajia kufanyiwa upasuaji wa kubadilisha nyonga ambapo pia itatumika kama sehemu ya kuwajengea uwezo wa umahiri madaktari wazawa.

“Nashukuru kwa kuja kwenu, mjisikie mko nyumbani na iwapo mtapata changamoto yeyote msisite kuwasiliana nasi, uwepo wenu hapa ni wa umuhimu kwetu, tunaahidi kuendeleza ushirikiano huu muhimu kwa ustawi wa maendeleo ya tiba hapa MOI” amesema Prof. Makubi 

Kwa upande wake kiongozi wa wataalam hao kutoka Pakistan Abdullah Amjad ameushukuru uongozi wa MOI kwa mapokezi mazuri, ukarimu na ushirikiano walioupata.

“Tunashukuru kwa mapokezi  mazuri, na tunaahidi kuendeleza ushirikiano huu mzuri” amesema Amjad

Mkurugenzi wa Huduma za Upasuaji Mifupa, Nyonga na Magoti Dkt. Athony Assey amesema kambi hiyo imeanza kwa upasuaji wa wagongwa wawili na baadae kuendelea na wengine hadi Machi, 01, 2024 kambi hiyo itakapomalizika.

Kambi hii ni matokeo ya jitihada za Serikali ya awamu ya sita baada ya kuiwezesha MOI kuwa na vipandikizi vyakutosha (Implants) ambapo hapo awali wagonjwa walisubiri huduma hii muda mrefu kutokana  na uhaba wa vifaa.

Post a Comment

0 Comments