Na AMEDEUS SOMI,
DAR ES SALAAM
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Jerry William Silaa amesema serikali ipo katika mchakato wa mwisho ili kutumia mifumo ya Tehema katika kutatua changamoto za ardhi katika mkoa wa Dar es Salaam na mikoa yote nchini.
Waziri Silaa amesema mfumo huo wa Tehema unaandaliwa ili
kurahisisha utendaji kazi katika kutatua changamoto za masuala ya ardhi Pamoja na
usaidizi mbalimbali wa ardhi nchini.
“Tunayo timu kubwa ya wataalamu pale Arusha inayoanda mfumo ambayo Mheshimiwa Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan ametenga fedha na ametuwezesha na ametuelekeza kwahiyo upo mfumo wa Tehama unaandaliwa mfumo ambao kesho hatutakuwa na marundo ya watu wanaokusanyika chini ya Maturubai wakifanya miamala ya ardhi, ukitaka kununua ardhi ukitaka kuomba hati utaingia kwenye simu janja yako utafanya miamala ya ardhi na itakamilika kwa muda mchahe na hatukakuwa na nafasi tena ya Waziri kuja kusolve tatizo ambalo linawez kutatuliwa na mfumo wa Tehema”
Katika hatua nyingine Waziri Silaa amewaasa wananchi kuwa na
mazoea ya kuandika mirathi ili kuepuka madhila yatokanayo na ugawaji wa mali
pindi mtu anapofariki.
“Nimeendelea kuziomba kuzisihi na kusisitiza familia zetu wale ambao wamejaliwa na Mwenyezi MUNGU Kuwa na Imani za Dini ambao wanaamini kuna kufa basi waandike wosia ili wapunguze usumbufu baada ya wao Kwenda mbela za haki, Binadamu yoyote anapofariki ni lazima mirathi ifunguliwe mali zigawiwe na mirathi ifungwe tunaendelea kuwasisitiza Watanzania kuendelea kufungua mirathi ya watu waliotangulia mbele za haki”
Akitoa tathmini ya kliniki za ardhi za nchi nzima amesema tayari
wamewaelekeza maafisa na makamishna wote wa ardhi kwa ngazi za mikoa na wilaya watoke maofisini
na Kwenda kutatua ero za ardhi kwa wananchi.
Kliniki hiyo ya Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya
Makazi mpaka sasa imeshafanya utatuzi, urasimishaji na utoaji wa hati katika
mikoa mbalimbali ikiwemo Dodoma inatarajia kumaliza Februari 25 katika Jiji la Dar es Salaam ambapo mpaka sasa
tayari imeshatoa zaidi ya Hati elfu saba itaelekea katika Majiji ya Tanga,
Mbeya, Arusha na Mwanza.
Joseph Edmund Mkazi wa Bunju ambaye amepatiwa Hati yake leo hii katika Kliniki hiyo |
BOFYA HAPA KUONA VIDEO
0 Comments