Na AMEDEUS SOMI,
DAR ES SALAAM.
Balozi Shaibu Said Musa Naibu
Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki amesema
sanamu ya Hayati Mwalimu Nyerere imefanana kwa asilimia 92 na uhalisia wa
Mwalimu Nyerere.
Akizungumza na Wahariri
pamoja na Waandishi wa Vyombo mbalimbali waliohudhuria mkutano ulioandaliwa na
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu Jijini Dar es Salaam, tarehe 22
Februari, 2024 amesema Serikali imefata maelezo ya kitaalamu iliyotolewa
na Kamati Maalum ambayo ilishiriki tangu mijadala mpaka kupatikana kwa ile sanamu
ambayo imefadhiliwa na Umoja wa Maendeleo Kusini mwa Afrika SADEC kwa wazo
ambalo lilitolewa na Viongozi mbalimbali wa Afrika ikiwemo Hayati Robert Mugabe
enzi za uhai wake.
“Kuhusiana na sanamu kweli kumekua na mixfillings na reactions ambazo wapo wanasema kwamba kuna hitilafu lakini nataka mjue tu kwamba upande mmoja wana mawazo hayo lakini wapo wengine upande wa pili wapo wenye kukubali na kusema kwamba ni Mwalimu Nyerere.
Aidha Balozi Said Mussa amesema Mtoto wa Hayati Nyerere
Madaraka Nyerere naye alikuwepo katika uzinduzi ule ambapo alisema kuwa sanamu
ile inafanana kabisa na baba yake na kama mtu anataka kujua Zaidi amtafute na
kumuuliza.
“Mwalimu mnayemuona katika sanamu ile ya Addis ni wa miaka ya 60-80 akiwa yupo Active katika mapambano ya kusaidia kuleta uhuru na maendeleo ya nchi za kusini mwa Afrika”.
“Kauli ya mwanaye ameendelea kusisitiza kwamba yule ni baba yake na kama kuna mtu anataka amtafute amuulize”
Taratibu za kitaalamu zinasema kwamba inatakiwa uipatie
angalau asilimia 75 ya sanamu unayoitengeneza katika utengenezaji wake na ile sanamu
ya Addis (Mwalimu Nyerere) ni asilimia 92.
0 Comments