Na Mwandishi Wetu,
DAR ES SALAAM.
Rais mstaafu wa awamu ya pili Mzee Ali Hassan Mwinyi amefariki dunia leo hii Alhamisi Februari 29 katika hospitali ya Mzena iliyopo Jijini Dar es Salaam.
Akitoa taarifa ya kifo chake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan amesema kifo chake kimetokana na ugonjwa wa saratani na atazikwa Jumamosi Machi 2 2024.
Rais ametangaza siku saba za maombolezo ambapo bendera zitapepea nusu mlingoti.
0 Comments