HEADLINES

6/recent/ticker-posts

MWILI WA EDWARD LOWASSA WAZIKWA LEO



Na AMEDEUS SOMI,

MONDULI ARUSHA.

Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Zamani wa Jimbo la Monduli (CCM) Hayati Edward Lowassa anazikwa leo Nyumbani kwake, Monduli, Mazishi haya yamehudhuriwa na viongozi wakuu wa Nchi wakiongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan.

Waombolezaji wametoa Salamu za Mwisho kwenye Jeneza la Hayati Lowassa, wakiongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, kisha famili ya Lowassa, viongozi wengine wa kitaifa pamoja na Viongozi waandamizi kutoka vyama vya upinzani, Freeman Mbowe na Zitto Kabwe.


Mazishi haya yataendeshwa kwa Sehemu mbili, Kidini na Kiserikali. Kwa upande wa Dini, Askofu Mkuu wa KKKT, Dkt. Alex Malasusa ataongoza ibada hiyo, kisha Jeshi la Wananchi la Tanzania litashiriki sehemu ya pili ya Mazishi hayo.

Kwa mujibu wa taratibu za Kijeshi, Hayati Lowassa amepigiwa Mizinga 17 kwa heshima yake.

Saa 6:25 Mchana, Maafisa wa JWTZ wenye cheo cha Kanali wanauingiza Mwili wa Hayati Lowassa Kaburini. Zoezi hili limefuatiwa  na kuweka udongo kaburini kama sehemu ya kuaga.

Saa 6:55 Mchana, maafisa wa JWTZ  ndio waliokufunika kaburi la Marehemu Edward Ngoyai Lowassa.

Mwisho sisi kama Familia ya Tupo Digital tunatoa pole kwa Familia, Jamii na watu wote wa Edward Lowassa.

Post a Comment

0 Comments