Na AMEDEUS SOMI,
DAR ES SALAAM.
Kliniki ya kurasimisha, kutatua na kutoa Hati imeingia
katika siku ya pili katika Kata ya Bunju na mpaka sasa tayari imeshatoa hati zaidi
ya elfu saba katika Jiji la Dar es Salaam.
Wakizungumza katika Kliniki hiyo iliyoandaliwa na Wizara ya
Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Ardhi wananchi wa Bunju katika Kata ya Wazo wameshukuru Serikali kwa
kuwasaidia katika kufanikisha kuwapatia Hatimiliki za viwanja vyao.
Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Nyumba na
Maendeleo ya Makazi Lucy Kabiemera amesema kama Wizara ya Ardhi wamekuja na
kampeni maalum ya kutoa hatimiliki za pamoja (Mke na Mume) ambapo hii itasaidia
kuongezeka kwa viwango vya umiliki wa ardhi kwa wanandoa.
“Baada ya kutoa hii hamasa hatimiliki walizotoa zaidi ya elfu saba kwa asilimia kumi zinamilikiwa na milki ya Pamoja yaani wanandoa”
Naibu Katibu Mkuu huyo amesema lengo la kuanzisha Kampeni
hiyo ni kupunguza migogoro ya mirathi pindi mmoja anapofariki.
Amewasihi wananchi kuchukua hati ya pamoja ili kuepusha
migogoro ya mirathi isitokee kwa baadae pindi mmoja anapofariki kwani hali hii huchangia migogoro
mingi ya ardhi na mirathi.
Kliniki hiyo inatarajia kuhamia katika mikoa ya Mwanza, Mbeya,
Arusha na Tanga.
BOFYA HAPA KUONA VIDEO
0 Comments