HEADLINES

6/recent/ticker-posts

HAFLA UWEKAJI JIWE LA MSINGI MRADI WA MAJI TANGA

Na Mwandishi Wetu,
TANGA.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango amezindua hati fungani ya kijani ya miundombinu ya maji Mkoani Tanga ambao utasaidia kwenye Sekta ya Afya ikiwa ni pamoja na huduma za Afya ya Uzazi mama na mtoto. 

Pamoja na mambo mengine pia Makamu wa Rais ameweka Jiwe la Msingi katika mradi mkubwa wa maji wa Mowe ulipo Jijini Tanga.

Uzinduzi huo umefanyika leo Februari 22, 2024 kwa jitihada za Mbunge wa Jimbo la Tanga Mjini Mhe. Ummy Mwalimu ambapo mradi huo utaongeza upatikanaji wa maji kwa wastani wa lita Milioni 15 inakua jumla ya upatikanaji wa maji lita Milioni 60 katika Jiji la Tanga Mjini, Wilaya jirani za Muheza na Mkinga baada ya lita 45 za awali. 

Mradi huo umeanza baada ya uzinduzi wa hati fungani ya Kijani ya Miundombinu ya Maji Tanga Katika eneo la Mabayani Jijini Tanga siku ya jana ukiwa na lengo la uboreshaji wa upatikanaji wa maji wenye gharama zaidi ya Bilioni 53 ambao utazalisha lita milioni 60 kwa Mkoa wa Tanga.

Waziri wa Afya na Mbunge wa Jimbo la Tanga Mjini Ummy Mwalimu akisalimiana na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Dkt. Philip Isdor Mpango wakati akizinduzia hati fungani ya kijani ya miundombinu ya maji Mkoani Tanga ambao utasaidia kwenye Sekta ya Afya ikiwa ni pamoja na huduma za Afya ya Uzazi mama na mtoto.




Post a Comment

0 Comments