HEADLINES

6/recent/ticker-posts

MBOWE ASHANGAZWA CHADEMA KUTOTAJWA HISTORIA YA LOWASSA, SAMIA AMJIBU

Na AMEDEUS SOMI,
Monduli ARUSHA.

Kwa dakika chini ya 7 alizotumia Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema Freeman Mbowe ameshangazwa na historia ya Waziri Mkuu mstaafu Marehemu Edward Ngoyai Lowassa aliyezikwa nyumbani kwake Monduli leo.

Mbowe amesema ameshangazwa kutotajwa Chama chake cha Chadema katika historia hiyo akisema huwezi kutaja historia ya kiongozi huyo pasipo kutaja Chama cha Chadema ambapo alikua mgombea Urais pekee wa Chama cha upinzani ambaye alijenga demokrasia kwa viwango ambavyo havijawahi kufikiwa na mgombea  mwingine yoyote wa upinzani katika Taifa la Tanzania.

“Kwa sababu ya rekodi niweke kumbukumbu sahihi,  huwezi kuiandika Historia ya Mheshimiwa  Lowassa ukaliacha neno CHADEMA, huwezi ni kujidanganya tu na kujaribu kuua historia ambayo huwezi kuiua kwahiyo nimesikiliza na nimeisoma sana historia ya Hayati Lowassa Nimesikiliza na kusoma sana historia ya Lowassa kama ambavyo imewasilishwa.

Mimi binafsi ni mtu mkweli na nimesikitika kwa sababu kwa kweli amefanya mambo mengi makubwa ndani ya serikali ndani  Chama cha Mapinduzi, ndani ya vyama vya upinzani  na katika Taifa letu na taifa hili ni letu sote.

Unawezaje ukaiandika historia ya  Mheshimiwa Hayati Lowassa ukasahau utumishi wake wa miaka minne kama mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema kama mgombea Urais wa Chadema wa mwaka 2015 ambaye alijenga demokrasia kwa viwango ambavyo havijawahi kufikiwa na mgombea  mwingine yoyote wa upinzani katika taifa letu?.

Nimeona niliseme hili kwa sababu taifa letu hili ni letu sote kwa sababu Mheshimiwa Rais na viongozi wote wakuu wapo pale.’’.

Aidha Kiongozi huyo wa Chadema amemwagia sifa kedekede marehemu Lowassa kwa kusema kuwa Lowasa ndie aliyekua mgombea urais ambaye aliwezesha kupatikana kwa Madiwani zaidi ya 2000 katika vyama mbalimbali vya upinzani nchini.

“Mheshimiwa Lowassa naye alikuwa ni mhanga wa mambo ya Uchaguzi, naamini (the Full Potential) ya Lowassa haikuwahitumika, haikuwahipatikana’’

Amemaliza Mbowe katika salamu zake za rambirambi.


Kwa upande wake Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan wakati akiwasilisha salamu zake za rambirambi pamoja na mambo mengine amesema kitendo cha Marehemu Lowassa kupata kura nyingi katika Uchaguzi Mkuu wa 2015 kilisababishwa na umaarufu wake mwenyewe aliokua nao katika Siasa.

''Lowassa alikua kiongozi aliyelea vijana wengi ambao wanaendelea kulitumikia Taifa sifa hii ya ulezi na kuongoza vijana katika maisha yao ya kisiasa ilimjengea umaarufu na mapenzi makubwa miongoni mwa wengi na ndio maana alichosema mdogo wangu Freeman yale matokeo ya zile kura ni kwa sababu hii alijenga umaarufu mkubwa sana yeye mwenyewe binafsi na ndio maana yamekuja.

Lakini pia tungeyasema sisi usingepata la kusema ndugu yangu na ndio maana mmekuja ili mpate la kusema kwahiyo nakushukuru sana mdogo wangu''

Post a Comment

0 Comments