HEADLINES

6/recent/ticker-posts

ZIARA YA MAKONDA YAONDOKA NA MKURUGENZI PANGANI


 Na Mwandishi Wetu,

Ziara ya siku ya mbili ya Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM, Paul Makonda mkoani Tanga imeondoka na mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Pangani mkoani hapa baada ya kusimamishwa akidaiwa kushindwa kutekeleza majukumu yake.

Taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Rais (Tamisemi), imeeleza kuwa Waziri wa wizara hiyo, Mohamed Mchengerwa amefikia uamuzi huo baada ya Mbenje kushindwa kutimiza majukumu yake, hivyo amewekwa pembeni ili kupisha uchunguzi.


Mchengerwa amesema katika taarifa hiyo kwamba Mbenje amelegalega katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo.
Kutokana na hatua hiyo, Mchengerwa amemwagiza Katibu Mkuu wa Tamisemi, Adolf Ndunguru kutuma timu ya uchunguzi katika halmashauri hiyo.

Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM Paul Makonda akizungumza na wananchi wa Pangani Jijini Tanga

Dalili za kusimamishwa kwa Mbenje zilionekana mapema jana Jumamosi Januari 20, 2024 katika mkutano wa hadhara uliofanyika wilayani humo, ambapo Makonda alieleza kutoridhishwa na utendaji kazi wa mkurugenzi huyo naayelalamikiwa na wananchi wa halmashauri hiyo.


Makonda alisema jana alipotembelea Pangani, alibaini kuna migogoro inayosababishwa na Mbenje aliyedaiwa kuwa ameshindwa kutimiza majukumu yake ya kuwahudumia na kutatua kero za wananchi wa wilaya hiyo.

Kutokana na hali hiyo, Makonda alimpigia simu Waziri Mchengerwa kumweleza kuwa mapendekezo ya CCM ni mkurugenzi huyo asimamishwe kazi na kuunda kamati ya kuchunguza malalamiko dhidi yake.

Post a Comment

0 Comments