HEADLINES

6/recent/ticker-posts

WAZIRI UMMY AWASILISHA TAARIFA UIMARISHAJI HUDUMA ZA AFYA


 Na Mwandishi Wetu

Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu amewasilisha Taarifa ya Uimarishaji wa Huduma za Matibabu ya Kibingwa na Ubingwa Bobezi kwa Kipindi cha Mwaka 2021 hadi 2024 kwenye Kamati ya kudumu ya Bunge ya Afya na Masuala ya UKIMWI ikiongozwa na Mwenyekiti wake Mhe. Staslaus Nyongo. 

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt.Grace Magembe

Waziri Ummy amewasilisha taarifa hiyo leo Januari 22, 2024 ambapo ametaja Baadhi ya huduma za ubingwa na ubingwa bobezi zinazotolewa na Hospitali Maalum, Kanda na Taifa ambazo ni pamoja na Huduma za kibingwa za uchunguzi wa magonjwa pamoja na Huduma za kibingwa na ubingwa bobezi za tiba.

Waziri Ummy amesema, huduma za kibingwa na ubingwa bobezi zitaendelea kuratibiwa na Wizara ya Afya kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais TAMISEMI ili kuhakikisha fursa ya hizi huduma zinawafikia wananchi wote na hivyo kuhakikisha Serikali inawapunguzia gharama za kuzifuata huduma hizi mbali na maeneo wanayoishi.

Waziri Ummy ameambatana na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Grace Magembe, Mkurugenzi wa Huduma za Kinga Prof. Pascal Ruggajo pamoja na Wakurugenzi wa Taasisi zilizopo chini ya Wizara ya Afya ikiwemo JKCI, NIMR, MOI, MNH, NHIF na OCEAN ROAD.

Post a Comment

0 Comments