Na Amedeus Somi,
DAR ES SALAAM.
Serikali kupitia
Wizara ya Afya imeendesha kikao kazi kwa
waandishi wa habari ili kuwa na
uelewa juu ya magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele.
Kikao kazi hicho
ambacho kimeendeshwa na Mpango wa Taifa wa Magonjwa yaliyokuwa hayapewi
kipaumbele kimefanyika katika ukumbi wa
Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS).
Akizungumza
katika kikao kazi hicho Afisa mradi wa mpango huo kutoka Wizara ya Afya Dkt.
Isaack Njau amesema kama Magonjwa haya
ni Matende na Mabusha, Kichocho , Minyoo ya Tumbo n kibofu cha mkojo, Usubi na
Trakoma.
‘’Kama Wizara tumekuwa tukipambana nayo takribani miaka 20 iliyopita na tumeona ufanisi mkubwa kwenye ugonjwa wa matende na mabusha maambukizi yamepungua kwenye Wilaya 112 ambapo hatumezeshi tena kinga tiba tumebakiwa na Wilaya 7 tu na Trakoma tumebaki na Halmashauri 9’’
Aidha Dkt. Njau ameendelea kusema kuwa katika ugonjwa wa kichocho na minyoo ya tumbo wameweza kupunguza maambukizi kwenye baadhi ya Kata na sasa wanatoa dawa pale ambapo maambukizi yanaonekana kuzidi.
Magonjwa haya
yanapatikana kwa kiwango kikubwa katika baadji ya maeneo mfano ugonjwa wa
kichocho upo zaidi katika mikoa ya kanda ya Ziwa na Ugonjwa wa Matende
unapatikana zaidi katika mikoa ya Pwani, kama Dar es Salaam, Tanga, Pwani na
Lindi.
Kwa upande wake Mratibu wa
magonjwa hayo kutoka Wizara ya afya Dkt. Clara Mwansasu amesema kabla ya kuanza
utekelezaji wa afua za magonjwa hayo kama Wizara walifanya tathmini na kugundua
magonjwa haya yameenea katika maeneo mbalimbali nchini kutokana na viashiria
vyake.
‘’Matende na mabusha katika tathmini ya awali ulionekana umeenea katika halmashauri 119 hadi kufikia mwaka 2003 ni halmashauri 7 tu zimeendelea kuwa na ugonjwa huo na ugonjwa wa usubi umeonekana kushamiri katika Halmashauri 28 zenye ukanda wa mabonde na milima yenye vyanzo vya maji licha ya kuwa mpaka sasa maambukizi yameshuka kwa kiasi kikubwa’’
Dkt.Clara
ameongeza kuwa katika ugonjwa wa kichocho na minyoo ya tumbo wameweza kushusha
ukubwa wa tatizo ambapo kwa tathimi ya awali ulinea katika Halmashauri 184 japo
bado wanaendelea kufanya afua katika halmashauri zote ili kushusha ukubwa wa
tatizo.
Malengo ya kikao
kazi hicho ni kujenga uelewa kujua afua mbalimbali katika kutokomeza magonjwa
hayo, waandishi wa habari kuwa na uelewa
sahihi wa kiutoa taarifa za maonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele
Kaulimbiu ya Mpango huo ni Tuungane tuchukue
hatua tutokomeze magonjwa yaliyokua hayapewi kipaumbele.
Maadhimisho ya siku ya magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele yatafikia kilele 30 Januari mwezi huu.
Kinachofanywa na Wizara kwa sasa ni umezeshaji wa
kingatiba kwa walengwa
Kuboresha usafi
wa mazingira
Huduma za
matibabu kwa walioathirika.
Kupambana na
wadudu waenezao magonjwa ya kuambukiza
Kutoa elimu kuhusu kushiriki na kupambana na magonjwa haya.
0 Comments