HEADLINES

6/recent/ticker-posts

TANZANIA NA INDONESIA KUSAINI HATI SABA ZA MAKUBALIANO


 Na Amedeus Somi,
DAR ES SALAAM,

Rais Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuanza Ziara ya Kitaifa nchini Indonesia kuanzia Januari 22 hadi 24 katika hatua ya kukuza uhusiano wa kidiplomasia na kuibua fursa za uwekezaji zitakazowanufaisha wananchi wa Tanzania.

Hati hizo za makubaliano zitahusisha sekta ya nishati, afya, Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), Shirika la Petroli Tanzania (TPDC), Kampuni ya Taifa ya Mafuta na Gesi ya Indonesia (PERTAMINA), Shirika la Madini nchini (STAMICO) kati ya zile zitakazonufaika.

Waziri wa Mambo ya Nje January Makamba akizungumza na Waandishi wa Habari katika ofisi ndogo za Wizara hiyo Jijini Dar es Salaam (Picha na Amedeus Somi)


Sekta nyingine zitakazonufaika ni pamoja na sekta ya kilimo, mifugo, uvuvi, uchumi wa buluu, elimu, utalii na sekta ya ulinzi.

Uhusiano wa kidoplomasia kati ya Tanzania na Indonesia umetimiza miaka 60 sasa tangu uasisiwe na marais wa nchi hizi mbili Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Rais Achmed Soekarno mwaka 1964 na ubalozi wake kufunguliwa Tanzania mwaka huohuo.

Ziara hiyo ya Mheshimiwa Rais Samia ni mwitikio wa mwaliko wa Mheshimiwa Joko Widodo, Rais wa Jamhuri ya Indonesia.

Rais wa Indonesia Joko Widodo


Post a Comment

0 Comments