Na Mwandishi Wetu,
Rais wa Shirikisho la Kabumbu nchini Cameroon Samwel Eto’o amewajia juu wachezaji wa Timu ya Taifa hilo baada ya matokeo mabovu waliyopata katika mchezo wa kundi C dhidi ya Mabingwa watetezi wa Afcon Senegal.
Wadogo zangu wapendwa naelewa, wengi miongoni mwenu hamjazaliwa Cameroon wala hamjawahi kucheza vilabu vya Cameroon. Nyie mlizaliwa ulaya huko mna haki juu ya viongozi.
Mimi Cameroon ilinifundisha kwamba, napokuwa na timu ya taifa natakiwa kuwa mwanajeshi. Niwe tayari kukikabili kifo napopambania bendera.
Leo Cameroon inapitia fedhea sababu wachezaji wengi hawana upendo wa asilimia 💯 kwa taifa hili. Niwieni radhi kwa kujiongelea mimi kama mfano.
“Kwa ajili ya upendo nilionao kwa nchi yangu, nilikuwa na uwezo wa kucheza mechi mbili kwa siku moja. Niliwahi kufanya hivyo, "Roger Milla" aliwahi kufanya hivyo, pia hata "François Omam Biyick."
Unafikiri Cameroon ilikuwa ikitulipa zaidi ya vilabu tulivyokuwa tukichezea?! Hapana. Kuichezea Cameroon tulikuwa hatupati hata 1/10 ya kile tunacholipwa sehemu nyingine.
Kufa ukiipambania nchi yako, thamani yake inazidi pesa yoyote katika ulimwengu.
"Manga Onguene" alivunjika mguu akiipigania jezi ya Cameroon. Huyu alikuwa mtu hatari wakati wake, alikuwa mchezaji bora kuliko mimi. Licha ya kuvunjika mguu na kutelekezwa lakini bado aliendelea kuipa heshima nchi yetu.
Kitu nachokiona, tulifanya makosa kuwakabidhi bendera watu waliozaliwa nje ya Cameroon. Uzalendo kwa taifa upo mbali na hisia za mioyo yao. Hawana DNA na udongo wa Cameroon. Lakini baada ya Afcon kila kitu kitabadilika.
Tutahakikisha tunafanya kipimo cha uzalendo kwa kila kijana kabla ya kumvalisha jezi ya nchi yetu."
0 Comments