Na Amedeus Somi,
DAR ES SALAAM,
Mawasiliano ya
barabara ya Kunduchi Mtongani yamerejea kufuatia kukatika kwa kingo ya daraja
la mto Tegeta kutokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha katika maendeo
mbalimbali nchini.
Akizungumza
wakati wa ziara ya kukagua kazi ya kurejesha huduma kwa wananchi katika maeneo
yaliyoathirika na mvua jijini Dar es Salaam Naibu Waziri wa Ujenzi Mhandishi Godfrey Kasekenya amesema serikali
imejipanga kukabiliana na changamoto zinazojitokeza na kutoa wito kwa wakala wa
barabara nchini Tanroads kuendelea kufanya kazi kwa haraka ili kurudisha huduma
kwa wananchi.
"Nitoe tahadhari kwa Tanroads Mkoa kukagua hasa maeneo ya madaraja mnapoona kuna changamoto yoyote inayotokea ili kuokoa maisha ya vyombo na watu muwe haraka kutoa tahadhari kwa sababu nyie ndio mnajua hivyo tusione shida kuweka alama za tahadhari hakikisheni mnapita kila maeneo"
Aidha katika hatua nyingine Mhandisi Kasekenya ametoa wito kwa wananchi kuacha kujenga pembezoni mwa kingo za mito kwani kwa kufanya hivyo kunachangia kongezeka kwa njia za maji.
Kwa upande wake Mkuu wa kitengo cha Matengenezo wa Tanroads Mkoa wa Dar es Salaam Mhandisi Suzana Lucas amesema kazi kubwa iliyofanyika ni kujaza mawe na kuelekeza maji kurudi katika mkondo wake kwani wingi wa maji yaliyoambatana na magogo ndio kilichopelekea kukatika kwa tuta linalounganisha barabara na daraja.
Daraja la Kunduchi Mtongani ambalo lilipata madhara |
Ziara hiyo ya
Naibu Waziri wa Ujenzi imepita kukagua miundominu katika maeneo ya Jangwani,
Kinondoni Mkwajuni, Kunduchi Mtongani
Mbweni na Mpiji.
0 Comments