HEADLINES

6/recent/ticker-posts

GADIEL MICHAEL AULA AFRIKA KUSINI

Na Mwandishi Wetu,
AFRIKA  KUSINI

Beki wa kushoto Gadiel Michael amejiunga na klabu ya Cape Town Spurs ya nchini Afrika Kusini akitokea Singida Fountain Gate FC kwa mkopo wa miezi sita (6).
Gadiel ameungana tena na kocha Ernest Middendorp ambaye alimfundisha kwa siku chache akiwa Singida Fountain Gate kabla ya kutimkia Afrika Kusini.

Ikumbukwe kuwa Gadiel alishawahi kukiwasha katika Vilabu vya Simba sc na Yanga Afrika katika miaka kadhaa iliyopita.

Gadiel Michael akiwa Singida Fountain Gate

Mwishoni mwa msimu uliopita Gadiel aliachana na Mabingwa wa zamani wa Ligi Kuu ya Tanzania Simba sc kutoka katika mitaa ya Msimbazi na Bunju Jijini Dar es Salaam.
"Wachezaji wengi wazawa watafanikiwa kupitia Singida Fountain Gate".
Kauli ya Mseamji wa timu hiyo Hussein Massanza

Post a Comment

0 Comments