Na Mwandishi Wetu,
RUVUMA,
Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa amewasili Mkoani Ruvuma kwa ziara ya siku tatu, ambapo amepokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Labani Thomas, leo tarehe 24 Januari 2024.
Katika ziara hiyo, Waziri Bashungwa atakagua miundombinu ya barabara na madaraja mkoani humo ikiwa ni pamoja na barabara ya Lumecha - Kitanda - Londo -Kilosa kwa Mpepo - Ifakara - Lupilo, mradi wa Songea - Lutukira pamoja na Bypass, mradi wa Amani Makoro pamoja na barabara ya Ruanda - Ndumbi Port na Daraja la Ruhuhu.
0 Comments