Na Mwandishi Wetu,
DAR ES SALAAM,
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye (Mb) amefunga maonesho ya tatu ya kidijitali ya Afya na Ubunifu yaliyoandaliwa na Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi cha Muhimbili katika kampasi ya Mloganzila, Jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na Vyombo vya Habari mara baada ya kufunga mafunzo hayo Waziri Nape amesema maonesho hayo yamewakutanisha wadau mbalimbali ndani na nje ya Nchi ili kujadili namna TEHAMA inavyoweza kuboresha huduma za Afya.
Pia Waziri Nape amesema mazungumzo na mijadala iliyotokana na maonesho hayo itaendelea na kutumika kuboresha huduma ya Aya kwa kila mwananchi.
Waziri Nape amesema kumekuwa na shida ambayo hospitali zimekuwa na mifumo mingi na haisomani kiasi ambacho imechangia kuongezeka kwa gharama za matibabu kwa wananchi na tunataka kwa kupitia TEHAMA tuboreshe huduma hiyo ili mtu akienda kokote taarifa zake ziwepo
Waziri Nape ameeleza jitihada mbalimbali zinazofanyika chini ya Serikali ya Awamu ya Sita katika kufanya mifumo ya TEHAMA isomane ili kuweza kupunguza gharama kubwa ya matibabu kwa wananchi Pamoja na zile za uendeshaji.
Pia Waziri Nape amesema Kuna uwekezaji mkubwa umefanyika kwenye mkongo wa Taifa wa mawasiliano ambao ndo njia kuu ya kupeleka hizo taarifa na kuna mifumo kadhaa lazima itengenezwe ili taarifa ziwe pekee kwa kila mtu.
Katika hatua nyingine Waziri Nape amewashukuru Chuo Kikuu cha Muhimbili, wadau wa maendeleo pamoja na wadhamini kwa kuwezesha maonesho hayo.
Maonesho hayo ya siku mbali yalianza tarehe 16 Novemba, 2023 na kutamatishwa Tarehe 17 Novemba, 2023 katika kampasi ya Mloganzila katika chuo hicho kilichopo jijini Dar es Salaam.
0 Comments