HEADLINES

6/recent/ticker-posts

TAHADHARI MVUA KUBWA KUSHUKA NOVEMBA 15 - 18, 2023


 Na Mwandishi Wetu,

DAR ES SALAAM,

Baada ya mapumziko ya siku mbili, mvua kubwa za El Nino sasa zinarejea tena Jijini Dar es Salaam na zitanyesha kwa siku nne mfululizo kuanzia kesho Novemba 15 na zitaendelea hadi Jumamosi ya Novemba 18 mwaka huu.

Kwa mujibu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini TMA ni kwamba, mvua hizo mbali ya Dar es Salaam pia zitapiga katika mikoa ya Tanga, Pwani, Morogoro, Lindi, Visiwa vya Unguja na Pemba ikijumuisha visiwa vya Mafia.

Mikoa mingine itakayokumbwa na mvua hizo kwa Jumatano ya Novemba 15 ni Njombe na Ruvuma ambapo athari zaidi ikiwemo mafuriko na baadhi ya shughuli za kiuchumi kusimama zitajitokeza siku ya Ijumaa.

TMA pia imetahadharisha mvua hizo kuweza kuambatana na upepo mkali unaofikia kasi ya Kilometa 40 kwa saa na mawimbi makubwa yanayofikia mita mbili ukanda wa Pwani ya Kusini ya Bahari ya Hindi mikoa ya Lindi na Mtwara.



Post a Comment

0 Comments