HEADLINES

6/recent/ticker-posts

AKIWA KIFUNGONI HAJI MANARA ATEMA NYONGO ATUPA DONGO KWA RAIS KARIA


 

"Mpaka sasa sijui nimefungiwa miaka mingapi sijiu mia saba maana naamniwa hiyo adhabu yangu hata sijaanza kuitumikia.

Kwanza Rais  amesema mimi niliwahi kufungiwa miaka 7 yeye ndio akanifungulia sio vizuri kumuita mtu mzima muongo mimi nilifungiwa mwaka mmoja na yeye hakutengua hiyo adhabu ni Tarimba Abbas akiwa mwenyekiti wa kamati ya nidhamu nilikwenda kwa kufata procedure nikamwambia mimi sijapata nafasi ya kusikilizwa nikaandika barua Kamati ikakaa ikanifungulia baada ya kuona sina hatia lakini sio yeye.

Tatizo lenu ninyi ni uongo,  Shida kubwa ya  Simba sio Kocha , sio wachezaji ni uongo yaani mnajiongopea wenyewe hawa Watanzania walivyo hawa Waafrika walivyo ukiwaambia ukweli wakakuelewa ukweli wako ni rahisi zaidi kuwaongoza kuliko ukiwaambia uongo kwa muda mfupi ukitegemea mambo fulani yapite halafu baadae ukweli ujulikane umekwisha.


Ni lazima tubadilishe mifumo yetu ya kiutawala katika hizi Clubs tuache kupeana uongo, Leo tunajenga Uwanja Bunjuu, michango mnachangishana huyoo, mkienda pale baada ya Wiki Nyau, leo sijui tunamleta mchezaji Fulani huyu katoka sijui timu Fulani alikua bab kubwa.

Mimi nilikua naleta mbwembwe naweza nikawaambia Simba ni kubwa sana hapa hata aje Barcelona Messi,  Iniesta , natengeneza Motivation kwa Wachezaji na Mashabiki, kuna vitu vya msingi huwezi kuongopa kuna vitu unaweza kufanya Chupli kwa ajili ya kutengeneza Fanpage. 

Mimi nakwambia ukweli siku hizi watu hawaendi Uwanjani mimi nina mchango kwenye mpira wa  nchi hii. 

Nyie hivi tulivyowapiga hizi 5 mimi ningekua nafanya Press nyie wote mngezimia kila mwanasimba angejifungia chumbani asingesikiliza mtu yoyote sasa hiyo ndio shida kwahiyo hapo inaonekana huyu akifunguliwa huyu.

Naihusisha na Simba kwa sababu Rais, juzi …. Alimwambia  Rais  wan chi ….alisema  kwamba nasikia wewe ni  Simba"


Post a Comment

0 Comments