HEADLINES

6/recent/ticker-posts

WAZIRI KAIRUKI ATOA WITO KWA SHIRIKA LA UTALII DUNIANI KUZINGATIA USAWA WA UTOAJI AJIRA


 Na Mwandishi Wetu,

Waziri wa Maliasili na Utalii,  Angellah Jasmine Kairuki (Mb) ametoa wito kwa Shirika la Utalii Duniani (UNWTO) kuzingatia usawa katika kutoa ajira ikiwemo masuala ya kijinsia.

Wito huo umetolewa leo tarehe 16 Oktoba 2023, wakati akichangia mjadala katika Kikao cha Kamati ya Programu na Bajeti ya Shirika la Utalii Duniani, ambayo Tanzania ni mjumbe anayemaliza muda wake. Kikao hicho kimefanyika sambamba na Mkutano Mkuu wa 25 wa Shirika la Utalii Duniani ulioanza leo jijini Samarkand, Uzbekistan. 

Akichangia katika kikao hicho, Kairuki ameelezea utayari wa Tanzania kuendelea kufanya kazi na Shirika la Utalii Duniani hususan kupitia miradi inayotekelezwa na Shirika hilo.

Aidha,  Waziri aliwashukuru UNWTO na UNDP kwa kuwezesha na kutoa mafunzo ya Kutangaza Utalii kwa njia za Kidigitali kwa Wadau wa Chama cha Wasafirishaji Watalii Tanzania (TATO). Vilevile, alipongeza juhudi za Mashirika hayo katika kuandaa Mkakati utakaounganisha Utalii na maendeleo ya kiuchumi kwa wazawa.

Post a Comment

0 Comments