HEADLINES

6/recent/ticker-posts

RAIS MUSEVEN AKUTANA NA NAIBU WAZIRI MKUU WA TANZANIA


 Na Mwandishi Wetu,

KAMPALA,

Rais wa Jamhuri ya Uganda, Mhe. Yoweri Kaguta Museveni amekutana na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko Ikulu ya Entebbe nchini humo ili kupokea salamu za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu  Hassan kufuatia Sherehe za Miaka 61 ya Uhuru wa Nchi ya Uganda. 

Mhe. Rais Museveni ameishukuru Serikali ya Tanzania na kuongeza kuwa ushirikiano kati ya nchi hizo mbili umekuwa na mafanikio makubwa ya kihistoria na kiuchumi.

Kwa upande wake, Naibu Waziri Mkuu alikabidhi zawadi kwa Mhe. Rais Museveni kama njia ya kuthamini mchango na ushirikiano baina ya Tanzania na Uganda.

Ujumbe wa Tanzania ukiongozwa na Naibu Waziri Mkuu, Mhe. Dkt. Doto Biteko ukiwa kwenye mazungumzo na Mhe. Rais Yoweri  Museveni (hayupo pichani) Ikulu ya Entebbe nchini Uganda


Hafla hiyo ilihudhuriwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Stephen Byabato, Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki anayeshughulikia masuala ya jumuiya ya Afrika Mashariki, Mhe Balozi Stephen Mbundi pamoja na viongozi wengine kutoka ubalozi wa Tanzania nchini Uganda.

Post a Comment

0 Comments