Na Mwandishi Wetu,
MWANZA,
SHIRIKA la usimamizi wa mazingira na maendeleo (EMEDO) la Mwanza Nchini Tanzania kwa ushirikiano na Shirika la Wanaharakati wa Ubuntu wa mazingira nchini Kenya (NAAM Festival) wamezindua mradi maalum wa Sanaa unaoitwa "Sanaa Ziwani Nyanza", mradi utakaokuwa wa mafunzo na sanaa ya maonesho.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka NAAM Festival, Mradi huo unalenga kujenga ushirikiano kati ya wasanii na wadau wa sanaa, katika kuongeza ushirikiano kati ya sekta binafsi na ya kijamii katika tasnia ya Sanaa.
"Mradi huu unazinduliwa leo tarehe17, Oktoba 2023, kupitia warsha ya siku 10 ambayo inafanyika katika ofisi za EMEDO jijini hapa.
Wasanii 6, wanashiriki kwenye warsha hii, Lakini pia utaambatana na maonesho ya Sanaa 'Art exhibition' ambayo yatafanyika tarehe 28 Oktoba 2023." Imebainisha taarifa hiyo ya NAAM Festiv
Aidha, taarifa hiyo imeongeza kuwa, Mradi huo unaungwa mkono na Taasisi ya Nafasi Art Space kupitia msaada wa Ubalozi wa Uswizi nchini Tanzania, pamoja na Ubalozi wa Norway.
0 Comments