HEADLINES

6/recent/ticker-posts

POLISI DAR WAMTIA KOROKORONI ALIYEKASHIFU VIONGOZI SERIKALINI

 


Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limemkamata na linamuhoji kwa kina Selemani Agai Gaya (18) mkazi wa Kigamboni, kwa tuhuma za kutoa lugha ya matusi mtandaoni dhidi ya Viongozi wakuu wa Serikali  Tanzania kwa kutumia mitandao wa kijamii. 

Mtuhumiwa huyu amekamatwa  Julai 29, 2023, na wenzake wamekuwa  wakitengeneza maudhui za mtandaoni (video) na kuzisambaza kwenye mitandao ya kijamii zenye kuwatukana na kuwafedhehesha  viongozi wakuu wa Serikali katika akaunti zao za Tiktok.

Mtuhumiwa huyu atafikishwa Mahakamani haraka iwezekanavyo. 

Jeshi la Polisi linatoa onyo kali kwa mtu/ watu wanao toa lugha za matusi na fedheha kwa Viongozi wa Serikali kwa njia ya mtandao na njia nyingine yoyote, kuwa Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na mamlaka nyingine za kisheria limejipanga kuwafuatilia na kuwakamata, kuwahoji kwa kina kuhakikisha wanafikishwa haraka kwenye nyombo vya sheria. 

Katika hatua nyingine, Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam Julai 31, 2023 limewakamata watuhumiwa saba  akiwemo Amani Kipolo mkazi wa Vingunguti kwa tuhuma za kumshambulia na kumsababishia kifo Hadija Hamisi na kuwajeruhi watu wengine nane (8). 

Watuhumiwa hao wakiwa na wenzao wakiwa kwenye kundi waliwashambulia wananchi mtaani maeneo ya Vingunguti kwa lengo la kulipiza kisasi wakati wakitoka kuzimka mwenzao aliyefahamika kwa jina la Nurdin Bwino. 

Aidha, awali marehemu huyo Nurdin Bwino aliuwa kwa kushambuliwa na wananchi alipokuwa na wenzake sita wakiwa na visu na vifaa mbalimbali vya kuvunjia alipojaribu kuvunja nyumba moja usiku wa Julai 30, 2023. 

Imetolewa na ; 

Muliro J. MULIRO - SACP 

Kamanda wa Polisi 

Kanda Maalum ya Dar es Salaam 

Post a Comment

0 Comments