Na Mwandishi Wetu,
DAR ES SALAAM
Mafunzo hayo yanayofanyika kila mwaka nchini yenye lengo la kuwajenga uwezo Watendaji wa Kampuni za waendesha ghala, Wasimamizi wa Ghala, Meneja Dhamana pamoja na washiriki binafsi yamefunguliwa na Mkuu wa wilaya ya Ubungo Mhe. Hashim Komba leo Tarehe 28 Agosti 2023, katika ukumbi wa Kilimanjaro uliopo katika Uwanja wa Maonesho ya Sabasaba barabara ya Kilwa Jijini Dar es Salaam.
Akizungumza katika Mafunzo hayo, Mhe. Komba alieleza kuwa Mafunzo haya yanakwenda kuongeza heshima kwa watendaji wa ghala na kupelekea utoaji wa huduma bora kwa Wadau wote, vilevile ameitaka Bodi ya Usimamizi wa Stakabadhi za Ghala kuongeza matumizi ya TEHAMA katika utendaji ili kuendana na mabadiliko ya dunia.
Pia , mafunzo hayo yamehudhuriwa na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Stakabadhi za Ghala Bw. Asangye Bangu pamoja na Mkurugenzi wa huduma za uendeshaji wa Biashara kutoka Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) Bi. Mary Fidelis.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Stakabadhi za Ghala Bw. Asangye N. Bangu amesema kuwa lengo kubwa ni kuongeza tija katika ufanyaji kazi na matarajio ya mafunzo hayo ni kuhakikisha kazi zinafanywa kwa usahihi kwa kuzingatia sheria .
Aidha Mhe. Bangu ameongeza kuwa Bodi ya Udhibiti na Usimamizi wa Mfumo wa Stakabadhi za Ghala imejipanga kuona ambavyo watatekeleza shughuli zao za kiserikali pia wamejitaidi kuingiza bidhaa mbalimbali kadiri sheria ilivyo waruhusu kufanya hivyo, Washiriki waliojitokeza kupata mafunzo haya watapatiwa cheti cha kufudhu usimamizi wa shughuli za uendeshaji Ghala ambacho kitatambuliwa na Bodi ya Stakabadhi za Ghala.
0 Comments