Na Amedeus Somi
DAR ES SALAAM
Waziri wa Elimu na Sayansi na Teknolojia Mhe.Adolph Mkenda mapema leo hii ameagiza walimu pamoja na wafanyakazi wa Shule ya Modern Islamic ya Pwani kutimuliwa kazi kwa kuonyesha udanganyifu katika Mtihani wa Darasa la Saba iliyofanyika mwezi Septemba.
Hiyo imekuja kufuatia taarifa zilizosambaa za Mwanafunzi Itsam Suleiman aliyebadilishiwa namba yake ya Mtihani.
Akizungumza na waandishi wa Habari Mhe. Waziri amesema Baada ya Timu ya Uchunguzi iliyoundwa ikisaidiana na Jeshi la Polisi wamebaini uzembe kwa watumishi na wasimamizi wa Mitihani hiyo hivyo kama Wasimamizi wa Elimu wametoa Agizo la kufukuzwa kazi kwa Watumishi wote waliohusika pamoja na Walimu wa Shule hiyo.
“Chalinze Modern Islamic inafungiwa kuwa kituo cha mtihani kwa sasa
Kwa wale watumishi wa serikali tumewaandikia barua na nina imani watafukuzwa kazi
Mwenye shule na Waalimu wa Shule hiyo wafukuzwe kazi na kama wasipofukuzwa tutawasiliana na Kamishna wa Elimu wote wafukuzwe kazi
Pili waalimu hawa walikuwa wanafanya kazi shule binafsi wafukuzwe kazi la sivyo tunafutia usajili Shule hii”
Kilichofanywa na Wizara
Wizara Ilianza kwa mambo yafuatayo
Walianza na Mwanafunzi aliyebadilishiwa namba ya mtihani
Hatua
Kuwasiliana na kamati kufanya uchunguzi
Kuangalia script ya wataalm toka Jeshi la Polisi
Mtuhumiwa alifanya mitihani 5 kwa kutumia namba 40 somo la mwisho alitumia namba39.
Uchunguzi ulibaini watahiniwa 4 Walibadilishiwa. No
Justine abdallah 41
Kutumia namba 40
Jacob nassoro 40-41
Lailat 30-44
Mruma na 39-40
Dosari
Uzembe wa watumishi wafuatao
Mudy Elfance Mndelwa-Msimamizi Mkuu
Vitalis Kindole-Msimamizi
Amran Bakari Ramadhan (Mwl Mkuu)
Uchunguzi
Mwandiko wa mtaniniwa 33 umefanana na mtahiniwa namba 34
Mwandiko no 34 unafanana na mwandiko wa aliyetumia no 33
Mwandiko wa mtahiniwa no 39 unafanana na aliyefanya mtihani aliyefanya kwa no 43
Jumla ya watahiniwa 7 walibadilishiwa namba za Mitihani
Matokeo
Baraza limefanya marekebisho ya namba za kila mtahiniwa ili aweze kupata matokeo halali.
Limefanya marekebisho hayo kulingana na uchunguzi wa Jeshi la Polisi.
Mitihani
Mitihani ya Taifa ya Darasa la nne inatarajiwa kuanza
26 na 27 Oct
Mtihani wa Upimaji wa Kitaifa Kidato cha Pili
Jumla ya Shule 5288.
TAZAMA VIDEO HAPA CHINI
0 Comments