Na Amedeus Somi
DAR ES SALAAM
Klabu ya Simba Sport ya Jijini Dar es Salaam wameingia mkataba wa Miaka miwili na Kampuni ya Mo Assurance kwa ajili ya Bima za Afya ya matibabu kwa wachezaji pamoja na wafanyakazi wa Klabu hiyo.
Akizungumza katika mkutano na Waandishi wa habari Mtendaji Mkuu wa Simba Barbara Gonzalez amesema Bima hii itakuwa inahudumia Wachezaji,Benchi la Ufundi na Wafanyakazi wengine.Aidha amesema huduma hii itakuwa inatolewa kwa kila mfanyakazi na wategemezi wao wanne katika familia moja.
“Mo Assurance itakuwa ikitoa huduma za afya ikiwemo kulazwa,huduma za wajawazito Tunakwenda kuweka historia katika klabu yetu”.
Huduma hii itakuwa ikigharimu kiasi cha Shilingi za Kitanzania 250Million kwa mwaka.
TAZAMA VIDEO HAPA CHINI👇👇
0 Comments